Share

TPSF, Trademark East Africa wajazwa mamilioni ya kufadhili mikutano

Dar es Salaam. Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Trademark East Africa (TMEA) wamesaini mkataba wa makubaliano ya kufadhili mikutano ya kibiashara baina ya sekta binafsi na umma (PPDs).

Mkataba huo utagharimu Sh2.7 bilioni ndani ya miaka mitatu ambapo unatarajiwa kufikia mwisho Juni 2022.

Akizunguza wakati wa utiaji saini leo Jumatatu Juni 3, 2019, mkurugenzi wa Trademark Tanzania, John Ulanga amesema fedha hizo zitasaidia majadiliano ambayo yatajikita katika masuala ya biashara, usafirishaji, saera na sheria mbalimbali ambazo zitarahisisha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji.

“Tanzania ina fursa nyingi sana kibiashara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika mashariki kutokana na Jiografia yake ya kupakana na nchi sita zisizo na bandari, tunaamini fedha hizi zitasaidia mijadala ambayo itaifanya nchi kutumia vema fursa iliyopo,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema fedha hizo zitatatua changamoto ya uhaba wa fedha uliokuwa kikwazo kikubwa wakati wa kuandaa mijadala.

“Tukiwa na fedha hizi hata tafiti nyingi zitafanyika ili kujua tatizo kiundani kabla ya kupendekeza kwenye mijadala,” amesema.

Source: Mwananchi

Disclaimer: The views and opinions expressed in this article are those of the authors and do not necessarily reflect the official policy or position of TradeMark East Africa.

Stay updated

Our Projects are transforming Eastern Africa.

Learn More

Quick Contacts

Our Global Donors